Endapo unahitaji kusafiri wakati pasi yako imeisha muda na uliyoomba haijaletwa Ubalozini au kama pasipoti imepotea, au unarudi nyumbani kwa sababu zozote zile na huna pasipoti, Ubalozi unaweza kutoa Pasi ya Dharura. Matumizi ya pasipoti ya dharura ni kwa safari ya kwenda Tanzania tu.

Ili kupata pasi ya dharura inatakiwa viambatanisho vifuatavyo;

  • Jaza Fomu za kuomba pasi ya dharura
  • Ambatanisha ushahidi wa Uraia wako wa Tanzania – Kitambulisho kuonyesha kuwa wewe ni Mtanzania,
  • Ripoti ya Polisi kuonyesha kuwa ulitoa taarifa ya kupotea kwa pasipoti (iwe kwa lugha ya kiingereza)
  • Nakala ya Pasipoti iliyopotea kama unayo
  • Barua ya kujieleza kwa nini unataka hati ya dharura
  • Picha 2 za pasipoti

Malipo ya SEK. 300 pamoja na SEK 120 (Sweden) na SEK. 150 (Nchi zingine) kwa ajili ya kutuma kwa posta kama hukuja Ubalozini.