Ubalozi umepokea taarifa toka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) kuhusu usajili wa watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora).

Mamlaka imemteua Bi.Rose Mdami kuwa afisa atakae shughulikia masuala ya diaspora ndani ya mamlaka ya NIDA. Dawati hili litatoa huduma kwa haraka kwa diaspora katika jengo la Magereza lililopo katika barabara ya kivukoni mjini Dar es salaam.
Kwa maelezo zaidi wasiliana moja kwa moja na Bi.Rose Mdami kupitia namba +255 713 412871

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya  NIDA