NI MUHIMU KUJIRIDHISHA NA TAARIFA KABLA YA KUZITUMIA AU KUZISAMBAZA
Katika kipindi hiki cha hali ya hatari inayoendelea nchini Ukraini ni muhimu kwa Watanzania walio katika eneo na mipaka ya nchi hiyo kuwa makini.
- Epuka kufanya malipo ya fedha kwa ahadi ya huduma za uokoaji au usafiri.
- Epuka kutoa taarifa au maelezo binafsi ya aina yoyote kwa taasisi au mtu yeyote kabla ya kuhakiki urasmi wa taasisi husika.
- Ni muhimu kuhakiki taarifa zozote za msaada (bila kujali chanzo cha taarifa husika) kabla ya kuzitumia.
- Ni vema kuwasiliana na mamlaka rasmi za kiserikali kama Ofisi za Balozi zetu, Taasisi rasmi za kiserikali, au mamlaka za nchi uliyopo. 4.a. Mawasiliano ya Ubalozi wa Tanzania Uswidi (+46720494576) 4.b. Mawasiliano ya Ubalozi wa Tanzania Ujerumani(+4915215117558)
- Ni muhimu kufuatilia kwa ukaribu vyanzo rasmi vya taarifa, ikiwemo tovuti za Balozi zetu za Uswidi na Ujerumani.
ANGALIZO Kumbuka kwamba kusambaza taarifa zisizo sahihi (hasa katika hali ya hatari inayoendelea sasa) ni kinyume cha sheria za mataifa, na unaweza kushitakiwa kwa makosa ya jinai.
TAARIFA RASMI TOKA UBALOZI
Ubalozi umefungua ukurasa maalum kwa ajili ya taarifa zinazohusiana na Ukraini