KONGAMANO LA DIASPORA
KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA, ZANZIBAR, TAREHE 23-24 AGOSTI 2017 

Ubalozi wa Tanzania, Sweden umepokea barua kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuhusu 
Kongamano la Nnne la Diaspora litakalofanyika Zanzibar, Tarehe 23-24 AGOSTI 2017. 

Kongamano hili linaandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana no Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wo Baraza la Mapinduzi - Zanzibar.

Kongamano hilo litakuwa la nne (4) kufanyika Tanzania, katika mfululizo wa makongamano yaliyofanyika kuanzia mwaka 2014 hadi 2016; (mara mbili mjini Dar es Salaam na sasa itakuwa mara ya pili kufanyika Zanzibar). 

Kongomano hilo litakutanisha Diaspora na wadau mbalimbali wa maendeleo hapa nchini na kutoa nafasi ya Diaspora kutembelea mabanda na kujadili mada zenye kugusia biashara, utalii na fursa za uwekezaji. 

Wana diaspora, viongozi/wawakilishi mnaombwa kushiriki. Kwa taarifa zaidi na kujiandikisha kushiriki tafadhali wasilianeni na;

Bi. Tagy Daisy Mwakawago, 
Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
This e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it , This e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it au 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Zanzibar.