News Flash

As you probably realize, staying on Zanzibar (or any of Tanzania's islands) is generally a lot cheaper than being on safari. Don't forget to look at the options on Mafia Island also if any of your party are serious divers or snorkellers; Mafia doesn't have the same quality of beaches … but it's a lot quieter than Zanzibar, and can have a much more exclusive feel for a similar cost.
 
Home arrow News and Events arrow SIKU YA BIASHARA KIMATAIFA, GOTHERBURG
SIKU YA BIASHARA KIMATAIFA, GOTHERBURG Print E-mail

"INTERNATIONAL TRADE DAY, GÖTEBORG, SWEDEN" 28.02.2019  

Mh. Balozi Slaa na timu ya maafisa wengine wa Ubalozi walihudhuria Siku ya Biashara Kimataifa iliyofanyika katika mji wa Gothereburg Sweden. Mkutano unaofanyika kila mwaka uliandaliwa na "Swedish Chamber of Commerce" tawi la Magharibi.

 

 

Katika mkutano huu wanachama hujadili changamoto na fursa zilizopo katika biashara na Uwekezaji Kimataifa. Mwaka huu walijadili biashara za makampuni ya Sweden katika nchi ya Amerika, Ujerumani, Norway, Uingereza, China na Masoko mengine mapya.

 

Balozi Slaa akibadilisha mawazo na wafanya biashara wa Sweden 

 

Ilikuwa nafasi nzuri kwa Ubalozi wa Tanzania ukiongozwa na Balozi Slaa kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizoko Tanzania. Wenye makampuni magharibi ya Sweden pia walifurahi kuwa na mafasi ya ana kwa ana kuuliza fursa katika sekta wanazopenda kuwekeza. Zaidi ya makampuni 190, taasisi za biashara na benki yalihudhuria.

 

Timu ya Tanzania: Kutoka Kushoto ni Issa Kapande, Diaspora wa Kitanzania, Mjasiriamali na mwanachama wa Swedish Chamber of Commerce Juma Ndwatta, Afisa wa Ubalozi, Mh. Balozi Slaa, Nimco Kapande, Diapsora na Mjasiriamali, Dennis Nyström (Juma), Mkalimani (Kiswedi/Kiswahili), Bi Joyce Malipula na Agnes Mwaiselage wote Maafisa wa Ubalozi.

 

Ubalozi utaendeleza mazungumzo na makampuni yaliyoonyesha nia ya kuwekeza au kufanya biashara Tanzania  

 

Last Updated ( Monday, 04 March 2019 )
 
< Prev   Next >
© 2019 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.