News Flash

As you probably realize, staying on Zanzibar (or any of Tanzania's islands) is generally a lot cheaper than being on safari. Don't forget to look at the options on Mafia Island also if any of your party are serious divers or snorkellers; Mafia doesn't have the same quality of beaches … but it's a lot quieter than Zanzibar, and can have a much more exclusive feel for a similar cost.
 
Home arrow News and Events arrow ZIARA YA MH. MAHIGE FINLAND
ZIARA YA MH. MAHIGE FINLAND Print E-mail

Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi. Dr. Augustine Mahiga nchini Finland tarehe 25 -26 Februari 2019.

Angalia madhumuni ya ziara katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland hapa. Taarifa zaidi ni kama ilivyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania.

Chini ni picha za pamoja katika mikutano mbalimbali.

  

  Mh. Waziri Mahiga, ujumbe wake toka Tanzania na mwenyeji wake Balozi Slaa wakiwa katika mkutano na makampuni mbalimbali ya Finland tarehe 26/02/2019. Mkutano huu uliandaliwa na "Business Finland". 

Balozi Mahiga na ujumbe wake walipata fursa ya kuwa na Kikao na Rais Mtaafu wa Finland (1994 -200) na Mshindi wa "Nobel Peace Prize" 2008  Mh.  Martti Oiva Kalevi Ahtisaari (wa tatu kushoto). Mh. Ahtisaari aliwahi kuwa Balozi wa Finland Tanzania mwaka 1973 -1976/77.

 

Balozi Mahiga katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje, Finland, Mh.Timo Soini (wa tano toka kulia) akiwa na mwenyeji wake Balozi Dr. Willibrod Slaa, Balozi wa Tanzania katika Nchi za Nordic, Baltic na Ukraine na Balozi Pekka Hukka, Balozi wa Finland, Tanzania. 

 

 

 Balozi Mahiga na mwenyeji wake Balozi Slaa wakiwa katika mkutano na Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Finland.

 

Wakiwa katika chakula cha mchana walikuwa na mkutano wa Biashara na Spika wa Bunge la Finland, Maofisa wa Bunge na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Finland. 

Last Updated ( Monday, 04 March 2019 )
 
< Prev   Next >
© 2019 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.