News Flash

As you probably realize, staying on Zanzibar (or any of Tanzania's islands) is generally a lot cheaper than being on safari. Don't forget to look at the options on Mafia Island also if any of your party are serious divers or snorkellers; Mafia doesn't have the same quality of beaches … but it's a lot quieter than Zanzibar, and can have a much more exclusive feel for a similar cost.
 
Home arrow Tanzanians arrow Announcements arrow PASIPOTI MPYA ZA TANZANIA
PASIPOTI MPYA ZA TANZANIA Print E-mail
Kwa Jumuia ya Watanzania

YAH: UTARATIBU WA MAOMBl YA PASIPOTI MPYA YA KIELETRONIKIA YA TANZANIA KWA WAOMBAJI WA NDANI NA NJE YA TANZANIA 

Ubalozi wa Tanzania Sweden umepokea maelezo toka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Idara ya Uhamiaji juu ya Utaratibu wa maombi ya pasipoti mpya kama ifuatavyo:

"Idara ya Uhamiaji imeanza kutoa Pasipoti mpya za ki-elektronikia kwa watanzania kuanzia tarehe 31 Januari, 2018. Pasipoti za zamani zitaendelea kuwa halali kwa matumizi hadi ifikapo tarehe 31 Januari, 2020. Utaratibu mpya wa maombi kwa sasa utawahusu waombaji wa Pasipoti waliopo ndani ya nchi tu. 

Kwa waombaji waliopo nje ya nchi wataendelea na utaratibu wa zamani na kupewa Pasipoti za zamani mpaka hapo mitambo ya kuchukua alama za vidole itakaposimikwa kwenye Balozi zetu". 

Hivyo kwa taarifa hii watanzania manaoishi nchi za Nordic na Baltic mtaendelea kutumia pasi mlizonazo na mkiomba mpya mtapata kama hizi za zamani mpaka hapo Ubalozi utakapowezeshwa kupokea maombi ya pasi mpya.

Ukipata taarifa hii mwambie na mwingine!
 

UBALOZI WA TANZANIA 
STOCKHOLM, SWEDEN
Last Updated ( Wednesday, 14 February 2018 )
 
< Prev   Next >
© 2019 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.