News Flash

As you probably realize, staying on Zanzibar (or any of Tanzania's islands) is generally a lot cheaper than being on safari. Don't forget to look at the options on Mafia Island also if any of your party are serious divers or snorkellers; Mafia doesn't have the same quality of beaches … but it's a lot quieter than Zanzibar, and can have a much more exclusive feel for a similar cost.
 
Home arrow Tanzanians arrow Passports
Tanzanians - Passports Print E-mail

 (Plus Giro Nr.) 103 7471-8 Bank Identification Code (BIC/Swift) Address: NDEASESS and 

International Bank Account Number (IBAN): SE2895000099604210374718 

PASI MPYA / NEW PASSPORTS

Kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika, maafisa wa Ubalozi hawataweza kuwafuata waombaji katika nchi zote za Nordic na Baltic. Wote mnashauriwa kufika Ubalozini Stockholm Sweden kuwasilisha maombi yenu. Tunasikitika kwa usumbufu utakaowapata.

Pasipoti za sasa ni kwa matumizi ya mtu mmoja tu, watoto pia wanatakiwa kuwa na pasipoti na watafuata taratibu zote zinazohitajika za utoaji wa pasipoti mpya.

Utaratibu wa kuomba pasi mpya kwa mwombaji wa mara ya kwanza na kwa yule ambaye pasi ya zamani imekwisha ni kama ifuatavyo; 

NB: Kuepuka usumbufu tafadhali fanya miadi (appointment) na Ubalozi kabla ya kuja.

 

(A)   Maombi:

 

 • Mwombaji anatakiwa awasiliane na Ubalozi ili aweke miadi (appointment) 
 • Mwombaji atapewa fomu za kuombea pasipoti (CT 5AI) siku ya kuomba
 • Fomu itajazwa mbele ya afisa wa ubalozi. 
 • Maombi yote yatajazwa kwa HERUFI KUBWA
 • Mwombaji atachukuliwa alama za vidole na ofisi ya Ubalozi husika na kuweka saini yake katika fomu mbele ya Afisa anayeshughulikia pasipoti, kwa kutumia kalama maalum.

(B)  Viambatanisho

Mwombaji atahitajika kuleta;

 

 • Picha tano ( 5) 'passport size' (zenye urefu wa 4.5cm na upana 4cm) ambazo nyuma yake zinaonyesha rangi ya maji bahari (skyblue background).
 • Pasipoti ya Tanzania iliyokwisha - itakayotolewa nakala ya kurasa zinazohitajika na afisa hapa Ubalozni
 • Cheti halisi cha kuzaliwa na nakala ya pasi ya mzazi Mtanzania kama mwombaji ana umri chini ya miaka 18 (Kwa mwombaji wa mara ya kwanza).
 • Cheti halisi cha kuzaliwa, nakala ya cheti cha kuzaliwa wazazi au hati ya kujiandikisha kama wazazi au babu na bibi walihamia Tanzania kutoka nchi nyingine. 
 • Kama unabadili jina ambatanisha barua kueleza sababu na vyeti au hati kuonyesha kubadili jina kihalali (deed poll)
 • Risiti ya malipo ya ada ya pasipoti SEK. 600. Tafadhali lipia kabla ya kuja Ubalozini katika Akaunti namba ni (Plus Giro Nr.) 103 7471-8 (kwa walipaji Sweden). Walipaji nje ya Sweden watumie Bank Identification Code (BIC/Swift) Address: NDEASESS and International Bank Account Number (IBAN): SE2895000099604210374718 (bila kuacha nafasi). 

MUHIMU:

 

 • Ubalozi haupokei fedha taslim! 
 • Vyeti, hati au barua vilivyotolewa Nchi nyingine viambatanishwe na tafsiri yake kwa kiingereza

Maombi yatatumwa Makao Makuu ya Uhamiaji Dar es Salaam. Pasipoti zitakapokuwa tayari waombaji wataarifiwa kwa kuweka tangazo katika Tovuti ya Ubalozi. 

 

(C)  Hati ya Kusafiri ya dharura - Tafadhali angalia maelezo hapa chini.

 

INAWEZEKANA KUPATA PICHA ZA PASI HAPA ILA PIGA SIMU KUJUA KAMA WAMEFUNGUA

 

Alhassani Express

Photo to Pass and ID 

Valhallavägen 84

114 27 Stockholm

Tel: 086122357 

 

Iko karibu na Tekniska Högskolan (Kuna uhakika wa kuwakuta wako wazi)

 

Ian Johnson Foto 

Djursholmsvägen 33,

183 52 Täby, Sweden ‎  

+46 8 630 08 66   ‎  

www.ianjohnsonphoto.se 

 

Iko karibu na Ofisi ya Ubalozi (Haina uhakika mara nyingi panakuwa pamefunga)

 Back To The Top
-------------------------------------------------------------------------------------------------

 

 PASI ZA KUSAFIRI ZA DHARURA/EMERGENCY TRAVEL DOCUMENTS (ETD)

 Tanzanians who are travelling on emergency reasons can be provided with an emergency travel document. The emergency travel document (ETD) can enable them to travel only to Tanzania. Reasons for requesting an ETD can be:

Payment for an ETD is SEK 290.00* including postage (attach receipt of payment).

Other requirements are, 2 passport sized photos, evidence that the applicant is a Tanzanian, and a police report for lost passport.


Endapo unahitaji kusafiri wakati pasi yako imeisha muda na uliyoomba haijaletwa Ubalozini au kama pasipoti imepotea, au unarudi nyumbani kwa sababu zozote zile na huna pasipoti, Ubalozi unaweza kutoa Pasi ya Dharura. Matumizi ya pasipoti ya dharura ni kwa safari ya kwenda Tanzania tu. 

Ili kupata pasi ya dharura inatakiwa viambatanisho vifuatavyo;

 

 • Jaza Fomu za kuomba pasi ya dharura 
 • Ambatanisha ushahidi wa Uraia wako wa Tanzania - Kitambulisho chochote kinachoonyesha kuwa wewe ni Mtanzania, cheti cha kuzaliwa etc.
 • Ripoti ya Polisi kuonyesha kuwa ulitoa taarifa ya kupotea kwa pasipoti (iwe kwa lugha ya kiingereza)
 • Nakala ya Pasipoti iliyopotea kama unayo 
 • Barua ya kujieleza kwa nini unataka hati ya dharura
 • Picha 2 za pasipoti
 • Malipo ya SEK. 200 pamoja na SEK 90 kwa ajili ya kutuma kwa posta kama hukuja Ubalozini.

 


 Back To The Top
-------------------------------------------------------------------------------------------------
 
WATOTO KATIKA PASI (CHILD ENDORSEMENT)

Watoto wanatakiwa waombewe pasi zao. Majina ya watoto hayawekwi tena katika pasi ya mzazi. 

 Back To The Top
--------------------------------------------------------------------------------------------------
PASI ILIYOPOTEA (LOST PASSPORT)

A police report in English for the lost passport is required. A copy of the lost passport/ number and DN number for old passports, a receipt of payment for passport fee SEK 1100.00. Follow passport application process as above.

Mwombaji mwenye Pasi iliyopotea anatakiwa awe na ripoti ya polisi kwa lugha ya kiingereza. Awe na nakala ya pasi ya zamani au namba yake na DN namba toka pasi ya zamani ina saidia katika kupata kumbukumbu za mwombaji. Malipo kwa waliopoteza pasi ni SEK 1100.00. Maombi ya pasi mpya ni kama ilivyoelezwa hapo juu.

  Back To The Top
-------------------------------------------------------------------------------------------------
 
 KUBADILIKA JINA (CHANGE OF NAME)

 

Those wishing to change name for any reason e.g. marriage and therefore need to apply for a new passport bearing the new name. Come in person to the Embassy to make the application. Write a letter to explain why you want to change your name, attach supporting documents on change of name ( deed poll, marriage certificate etc.). Other attachments as listed above (fees and passport photos).

Ukihitaji kubadili jina kwa sababu yoyote ile kama ndoa inabidi uombe pasipoti mpya yenye jina jipya. Inabidi kuja Ubalozi kuomba. Andika barua ya kujieleza sababu ya kubadili na ambatanisha ushahidi wa kubadili aidha kwa ndoa au kwa kubadili kwa hiari uwe na hati ("deed poll", cheti cha ndoa nk).

All letters must be addressed to the Director of Immigration, U.F. S Embassy of Tanzania, Sweden. Barua iandikwe kwa Kamishana wa Uhamiaji, Dar es Salaam, K.K.K Ubalozi wa Tanzania Sweden.

  Back To The Top
-------------------------------------------------------------------------------------------------

 MALIPO (FEES)

 No. Type of Fee
 Amout of Fee in SEK
Postage  in SEK
 1. New passport

   600.00

        -
 2. Lost Passport (once)

 1100.00

         -
 3. Lost Passport (twice)

 1800.00

 
 4. Emergency Travel Document (ETD)

   200.00

        90.00
5. Renunciation of Tanzanian Citizenship

 1000 .00

        90.00
6. Endorsement and Legalisation of Documents

   200.00  per document

        90.00

 All fees are subject to change at any time.

Please make all payments (fees and postage) as indicated above  to:-

Näsby Allé 6, 183 55 Täby;
Tel: +46 8 732 24 30/1,
Fax: 46 8 732 24 32;
E mail: This e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it


Our Plusgirot Bank (Publ) Account Number 103 7471-8 (for paying customers within Sweden).

When payments are made outside Sweden, applicants can use the following: 

 • Bank Identification Code (BIC/Swift) Address: NDEASESS and
 • International Bank Account Number (IBAN): SE2895000099604210374718 (no space).

Payment is always in advance - credited to our Postgirot Bank and receipt of payment must be attached. Cheques are not acceptable.

Please ensure to send all attachments required in your application and a receipt or proof of payment of fee and postage (if not submitted personally).

 Back To The Top
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------
 
 PASI ZILIZOKAWIA

 

Ubalozi wa Tanzania Stockholm kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji Dar es Salaam Tanzania wanajitahidi kuhakikisha kuwa Watanzania wanaoishi katika nchi za Nordic na Baltic ambao walituma maombi ya pasi mpya za kusafiria na bado hawajazipokea mpaka sasa wanapatiwa pasi hizo mapema iwezekanavyo.

Pasi nyingi zinazokawia kutolewa ni kwa sababu maombi yanaupungufu. Tafadhali tunaomba mzingatie masharti na viambatanisho vinavyotakiwa. Waombaji wanaohitaji kuambatanisha vyeti vya kuzaliwa, ndoa, barua ya polisi, kubadili jina n.k tunawaomba walete tafsiri zake kwa kiingereza. Wale wanaoahidi kutuma baada ya kuambiwa upungufu tunawaomba watekeleze haraka la sivyo maombi yao yanawekwa pembeni.

Ikiwa viambatanisho vyote vimekamilika na pasi bado imekawia msisite kutupigia Ubalozini Na. +46 8 7322430/31au kutuma barua pepe mkitumia anuani This e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it . Katika taarifa hii tafadhali hakikisha unaleta:

 • Jina lako kamili,
 • Eneo unaloishi/Anuani, na
 • Tarehe uliyoleta maombi yako.

Ukipata taarifa hii tafadhali mweleze na mwingine!!!!!!!!!!

 Back To The Top
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------
 
PASI MPYA ZILIZOPOKELEWA UBALOZINI

 

Pasipoti, hati nk. zinapoletwa Ubalozini toka Uhamiaji tunazitangaza hapa. Kwa watanzania walioko Stockholm wanakaribishwa kuchukua wao wenyewe hapa Ubalozini. Kwa wale walioko nje ya Stockholm wahusika wanaombwa watume anuani zao za sasa kwa barua pepe ( This e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it ) ili tuweze kuwatumia kwa register. Kwa vile pasipoti ni muhimu ni vyema anuani ya muhusika anayotumia hivi sasa iandikwe kwa ufasaha ili kuzuia upotevu.

Wale ambao hawataona majina yao tunawaomba wawe na subira. Ikiwa utapatwa na dharura wakati ukisubiri pasi mpya, Ubalozi unaweza kutoa pasi ya dharura kwa safari ya kwenda Tanzania tu.

Majina yafuatayo ni kwa pasi au hati za kuukana uraia zilizotolewa na kutumwa hapa Ubalozini. 

PASIPOTI ILIZOPOKELEWA 14 JULY 2017 

1. ESHE SALEH MOHAMED 

PASIPOTI ZILIZOPOKELEWA 8 JUNE 2017 

1. MARYAM ALI KHAMIS ABDALLA

2. MARYAM ABDALLA ABILLAHI

3. SELINA ABIOLA SANYADE

4. MUNIR ALLY MOHAMED

 

PASIPOTI ZILIZOPOKELEWA 28 MAY 2017 

FAUSTINE HUGO MWAKAMELA     

ISAAC NAZARETH MWAMGOGWA     

MOSES BROWNE MWAKYANJALA     

SHANI RAJABU CHALLENGE     

DANIEL GETMAN SOLNES-MWANDWANGA     

HAWA HUSSEIN JUMALE     

MSILANGA PATRICK GEORGE MKANZABI     

YORAMU MKWASI KADUGU     

ROSE EDIMONDI LUNDBERG     

PETER EDMUNDI PIUS     

NORA ALEX MAKUMULI     

DINSMORE DICKSON MANGA     

ROSE BERNARD SEMNG'INDO ANDERSEN     

MWAJUMA DHAHARANI KYAZE     

MAGDALENA WENCESLAUS MACHIBYA     

GODFREY MOSES NDETALlO     

CHETI

1.   FEDA DOROTH MCHAINA 

 PASIPOTI ZILIZOPOKELEWA 02 MAY 2017

1.

SANTON BUBERWA MTENSA

2.

MEHDI ADILI AHMED

3.

JANE SAMWEL TYEAH

4.

ALICE SIYA MTUI

5.

NICE VINCENT CHUWA

6.

EVELYN GOSTA LUNDBERG

7.

ELISIFA SONGELAELI M. CARLISTEDT

8.

WENDE LUVINGA HEINOJA

9.

MARTHA MATHIAS BAHEMU

10.

ANNA BELLA GEFVERT

11.

TEDDY YAMWAKA STRUNGE

12.

JULIUS ALEWARYO MASSAWE

13. 

TAFI RAJAB HAMISI

14.  

SAPHIA ALLY ABDALLAH

15.  

BERNARD MANG'ANA P. GOSHASHY

 

 PASIPOTI ZILIZOPOKELEWA KABLA YA APRIL 2017

1. BETTY JOHN NYIKA  

2. PHILBERT MICHAEL NGOTI   

3. MARGARETH ALPHONCE TAWETE  

4. ELIBARIKI THADEO ELPHAS  

5. MUGASA MAGESA CHACHA

6. BOB FRANK TAYLOR  

7. JAYDA JENIFER IDRISSA KOROMA

8. ZUBER WILLIAM  KABADA  

9. VICKY JUMA   KAPAMA  

10. MELISSA NJUHI NDUNGU      

11 CLEOPHANCE VINCENT MWAULAMBO   

12 SALOME BERNARD TWEVE  

13 SOLOMON AARON MWAMBAPA  

14 AALIYAH ADAM MJEMA  

15 ADAM WILLIAM MJEMA  

16 PETER JACKSON NSHIMBA  

17 MOSSY NELL PAUL  

18 DIANA CHARLES MAKENE

19 SAMEER NASIR RAJAB   

20 HASSAN SAID HUSSEIN  

21. STACEY JOYCE MWANGAZA

22. GILLIAN SIMON BERGERSON

23. IBRAHIM KHAMIS MWINSHEHE

24. YUSUF MOHAMED NOOR

25. SHERINA SIMON RENDINI 

26. EDWARD MASHIKU NTEMI

27. MOHAMED MOHAMUD ABDUL WARSAME

28. AMELIA ADESUWA AGHAFEKOKHIA

29. DYLAN ERIC AGHAFEKOKHIA

30. ANNA GRACE NATASHA KATO

 

VYETI

1. ELIEKA NDETAIYWA GRAFTAS

2. JAMES MUNYANEZA APPOLINARY

3. VEILA BARSNES

4. TALIB NASSOR BAHAJ

5. KAREEEN DENNIS MAZALI

6. JULIANA JOHN SAMWELI

7. GLORIA PETER BIHAYI

8. SHAABAN SALUM OMAR

9. OMAR HASSAN MOHAMED

10. HAKIM ISLAM MAHDI AL-MASHJARY

11. ABDUL FAZALDIN IMAMDIN

12. ESHIDOREEN PATRIC ANIN NTENGA

13. COLIN PATRIC ANIN NTENGA

14.  ANWAR MAKELIO D'VAZ

15.  HALIMA YUSUPH AHMED

16.   ZAHRA AHMED NOOR

17. NURUHATUNI ALLY SALUM

 

PASIPOTI ZILIZOOKOTWA

 

1. TELIAN TANGIDI KALUNJU

2. ABDALLAH SALEH OMAR

3. RUSINA AHMED PIPINO

 

   Back To The Top----

 

Last Updated ( Friday, 14 July 2017 )
 
© 2017 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.