News Flash

As you probably realize, staying on Zanzibar (or any of Tanzania's islands) is generally a lot cheaper than being on safari. Don't forget to look at the options on Mafia Island also if any of your party are serious divers or snorkellers; Mafia doesn't have the same quality of beaches … but it's a lot quieter than Zanzibar, and can have a much more exclusive feel for a similar cost.
 
Home arrow Diaspora arrow THIRD DIASPORA CONFERENCE-ZANZIBAR
THIRD DIASPORA CONFERENCE-ZANZIBAR Print E-mail
MKUTANO WA TATU WA DIASPORA KUFANYIKA ZANZIBAR  TAREHE 24 – 25 AGOSTI, 2016

Ubalozi unapenda kuwafahamisha kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Utawala Bora- Zanzibar zinaandaa Kongomano la Diaspora (THIRD DIASPORA CONFERENCE) linalotarajiwa kufanyika tarehe 24 – 25 Agosti, 2016 katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort huko Mbweni, Zanzibar.
 
Kongamano hili litakuwa la tatu kufanyika katika mfululizo wa makongamano yaliofanyika mwaka 2014 na 2015 jijini Dar Es Salaam. Kongamano hilo litahusisha Diaspora na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini Tanzania.
 
Mgeni rasmi wa ufunguzi wa Kongamano anatarajiwa kuwa Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwa kama mwenyeji siku ya tarehe 24 Agosti 2016. Aidha, shughuli hiyo inatarajiwa kufungwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 25 Agosti, 2016.
 
Kongamano la mwaku huu lina Kauli Mbiu ya: “Bridging Tanzania Tourism and Investment: A New Outlook” na motto ya “Mtu Kwao ndio Ngao”. Kongamano litajikita katika kuhamasisha ushiriki wa Diaspora katika kuwekeza na kukuza biashara hapa nchini. Pamoja na shughuli za ufunguzi na kilele, matukio muhimu yatakuwa ni maonesho ya kibiashara, mada na majadiliano kuhusu ushirikishwaji wa Diaspora katika kuleta maendeleo Tanzania.
 
Washiriki wote watatakiwa kulipa Dola za Kimarekani sabini na tano (USD 75), kwa ajili ya ada ya ushiriki wa siku zote mbili za Kongamano; pamoja na chakula cha jioni (Gala Dinner).

Washiriki wanaweza kujiandikisha kupitia tovuti hii (http://www.tzdiaspora.org)

Watanzania wote wanaoishi katika nchi za Nordics na Baltics mnahimizwa kushiriki mkutano huo muhimu.
 

Last Updated ( Thursday, 28 July 2016 )
 
< Prev   Next >
© 2019 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.