News Flash

On his last day in Tanzania, President Clinton became one of 360, 000 visitors annually to explore the World Famous Ngorongoro Crater. Often called "Africa’s Eden" and the "8th Natural Wonder of the World," this collapsed volcano (a “caldera”) is located in the Ngorongoro Conservation Area . This is a natural sanctuary for thousands of birds, insects and animals such as lions, zebra, black rhino and wildebeest, all free to wander.
 
Home arrow Diaspora arrow KILIMANJARO DIASPORA AKAUNTI
KILIMANJARO DIASPORA AKAUNTI Print E-mail
TANGAZO - Kilimanjaro Diaspora Akaunti katika Benki ya Amana

Tunapenda kuwafahamisha kuwa Ubalozi umepokea barua kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikifahamisha kuhusu Akaunti Maalumu ilioanzishwa na Benki ya Amana kwa ajili ya Diaspora (Kilimanjaro Diaspora Account). Akaunti hiyo inaendeshwa kwa kufuata miongozo ya Dini ya Kiislamu( Sharia Compliance: Al Wadiah na Mudharabah contracts).
 
Ubalozi utatumika kuthibitisha nyaraka za kufungulia Akaunti (Verification of Documents) zitakazowasilishwa na wanaoishi eneo husika la uwakilishi kabla ya kuendelea na taratibu nyingine za kufungua akaunti hiyo. Uthibitisho huo ni muhimu kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kifedha nchini Tanzania.
 
Diaspora watakaopenda kufungua akaunti hiyo wanashauriwa kupakua  (download) fomu za kufungulia akaunti kupitia www.amanabank.co.tz/en/open-an-account/kilimanjaro-diaspora-account  na wakimaliza kujaza fomu hizo na kupitishwa na Ubalozi watatakiwa kuzituma kwa gharama zao kwenda anuani ya benki kwa njia za DHL, FedEx, EMs.
 
Wafunguaji wa akaunti wanaweza pia kuwasiliana na Benki ya Amana kwa simu namba +255 22 2129007  au kuongea moja kwa moja na Bw. Dasu Mussa, Meneja wa Masoko na Miradi (+255 786 687 832) au Bw. Muhsin Muhamed, Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Sharia (+255 653 283 636).
 
 
Ubalozi wa Tanzania
SWEDEN 
Last Updated ( Tuesday, 26 July 2016 )
 
< Prev   Next >
© 2019 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.