News Flash

On his last day in Tanzania, President Clinton became one of 360, 000 visitors annually to explore the World Famous Ngorongoro Crater. Often called "Africa’s Eden" and the "8th Natural Wonder of the World," this collapsed volcano (a “caldera”) is located in the Ngorongoro Conservation Area . This is a natural sanctuary for thousands of birds, insects and animals such as lions, zebra, black rhino and wildebeest, all free to wander.
 
Home arrow News and Events arrow Events arrow BI MATINDE MJASIRIAMALI, TANZANIA
BI MATINDE MJASIRIAMALI, TANZANIA Print E-mail

Bi.  Anna Matinde Atembelea Ubalozi wa Tanzania Sweden na Kukutana na Wanadiaspora.

Bibi Anna Matinde alikuwa Sweden kwa mwaliko wa Chamber Trade Sweden kuhudhuria Mkutano unaohusu Wanawake Wajasiliamali, Afrika. 
 
 
 
Bibi. Matinde ni mwanamke mjasiriamali pekee kati ya wanachama 11 wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi (Tanzania Private Sector Foudnation-TPSF), akiongoza kitengo cha Wanawake Wajasiriamali. TPSF inaongozwa na Bw. Reginald Mengi, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP.  Bibi Matinde pia ni Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccos iliyozinduliwa Dar es Salaam, Tanzania December 2014. TASWE - Saccoss inawawezesha Watanzania na wanachama kuweka akiba, kukopa na kununua hisa kwa ajili ya kupata mitaji ya kuboresha shughuli zao za kijamii na kiuchumi.
 
Tarehe 12 Aprili 2016, Bibi Matinde alitembelea Ubalozi wa Tanzania Stockholm na kuwa na mazungumzo na Mh. Balozi Dora Msechu.  
 
 
 Bibi Matinde alipokutana na Balozi Dora Msechu na Bw. Jacob Msekwa, Mkuu wa Utawala.

   
Tarehe 13/4/2016 Bi Matinde alikutana na Uongozi wa Jumuia ya Watanzania, TANRIK na wawakilishi wa wanawake wanadiaspora hapa Stockholm. Katika mikutano hiyo aliwafahamisha wanadiaspora fursa mbali mbali zilizopo nyumbani za wajasiriamali na wawekezaji wa nje. 
 
Aliwakaribisha watakaopenda kujiunga na Taswe Saccos ili waweze kuweka akiba, kukopa na kununua hisa kwa ajili ya kupata mitaji ya kuboresha shughuli zao za kijamii na kiuchumi huko nyumbani. Kwa maelezo zaidi na namna ya kuwa mwanachama tafadhali tembelea hapa: TASWE.
 

Bibi Matinde alipokutana na wanadiaspora wanawake waishio Stockholm, Sweden

Last Updated ( Monday, 16 May 2016 )
 
< Prev   Next >
© 2018 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.