News Flash

On his last day in Tanzania, President Clinton became one of 360, 000 visitors annually to explore the World Famous Ngorongoro Crater. Often called "Africa’s Eden" and the "8th Natural Wonder of the World," this collapsed volcano (a “caldera”) is located in the Ngorongoro Conservation Area . This is a natural sanctuary for thousands of birds, insects and animals such as lions, zebra, black rhino and wildebeest, all free to wander.
 
Home arrow News and Events arrow Events arrow WASANII WATEMBELEA SWEDEN
WASANII WATEMBELEA SWEDEN Print E-mail

WASANII WA MUZIKI WA TANZANIA WATEMBELEA

SWEDEN 2016.


Mwaka huu umekuwa wa bahati kwa Watanzania na marafiki wa Tanzania hapa Sweden kupata ugeni na burudani toka kwa wanamuziki watatu wa Bongo Flava na Jazz, Bi Sara Larsson, Naseeb Abdul Juma na Sauda Jasmine Simba. 
 
    
Sara Larsson  
   
  Naseeb Abdul Juma
 
Sauda Jasmine Simba. 

Bi. Sara ameishi sana Tanzania na ni mzaliwa wa Sweden lakini ni mwimbaji mahiri wa nyimbo za Kiswahili na anajulika kwa jina la kisanii kama SaraHa. SaraHa aliiweka Tanzania katika macho ya watazamaji wa muziki Sweden na Ulaya kwa ujumla aliposhiriki katika mashindano ya kutafuta Wimbo Bora Sweden "Melodifestvalen" mwezi wa Februari 2016. Wimbo alioimba unaitwa"Kizunguzungu".
 
 
Naseeb Abdul Juma ajulikanaye kama Diamond Platnumz naye alitumbuiza kwa mfululizo Ujerumani, Uholanzi, Ubelgiji, Norway, Sweden, Denmark na Finland mwishoni mwa Machi na mwanzo mwa Aprili 2016. Safari yake aliyoiita "From Tandale to the World Tour" ilikuwa ya kipekee kwani alisindikizwa na familia yake na timu nzima ya "Wasafi"

 
Diamond akiwa Sweden 
 
 
  
Diamond, timu yake na wenyeji wao Clay Onyango na Fortune Bernado

Bi Sauda Simba mwimbaji wa "Bongo Flava" na "Jazz" anayejulikana kwa jina la kisanii Sauda Jazzmin alitembelea Sweden mwezi April na kutumbuiza katika miji mbali mbali akishirikiana na waimbaji wa musiki wa Jazz wa hapa Sweden. Sauda Simba ni mwanamke Mchumi na Msanii mwenye vipaji vingi ikiwa ni pamoja na uandishi wa vitabu na uigizaji. Ziara yake Sweden ilikuwa sio tu kuimba ila pia kama Meneja wa miradi katika Nyumba ya Sanaa, Dar es Salaam, Tanzania unayogharamiwa na Swedish Institute. Alikuja kwa mwaliko wa Marafiki wa Nyumba ya Sanaa, Sweden. 
 
  
Bi Sauda Simba na mwenyeji wake Bi. Inger Thede, Msanifu wa jengo la Nyumba ya Sanaa, Dar es Salaam na Kaimu Mwenyekiti, Chama cha Marafiki wa Nyumba ya Sanaa.

 
Sauda Simba na Anders Linder wakiimba musiki wa Jazz Stockholm
 
Balozi wa Tanzania Mh. Dora Mmari Msechu aliwashukuru wasanii wote hao kwa kuitangaza Tanzania na kutoa Burudani kwa waliohudhuria Tamasha zao. Alipata nafasi ya kuhudhuria baadhi ya maonyesho na kutuma wawakilishi katika mengine. Aliwashukuru kibinafsi Bi Sauda Simba na Sara Larsson walipotembelea Ubalozi wa Tanzania Stockholm.
 
  
Bi. Sauda Simba  akiwa na Balozi Dora Msechu, Naibu Balozi Andy Mwandembwa na Mkuu wa Utawala, Jacob Msekwa.
 
 
 
Bi Sauda Simba katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, Sweden.
 
 
Bi. Sara Larsson alipotembelea Ubalozi wa Tanzania, Stockholm.

Last Updated ( Friday, 22 April 2016 )
 
< Prev   Next >
© 2019 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.