News Flash

On his last day in Tanzania, President Clinton became one of 360, 000 visitors annually to explore the World Famous Ngorongoro Crater. Often called "Africa’s Eden" and the "8th Natural Wonder of the World," this collapsed volcano (a “caldera”) is located in the Ngorongoro Conservation Area . This is a natural sanctuary for thousands of birds, insects and animals such as lions, zebra, black rhino and wildebeest, all free to wander.
 
Home arrow Tanzanians arrow Announcements arrow KUTOA MAONI - KATIBA MPYA
KUTOA MAONI - KATIBA MPYA Print E-mail

Ubalozi wa Tanzania, Sweden umepokea barua toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Tanzania ikiambatanisha mwongozo wa kutoa maoni juu ya katiba mpya kama ifuatavyo;

MWONGOZO KUHUSU UTARATIBU WA WATANZANIA WANAOISHI UGHAIBUNI KUTOA MAONI KUHUSU UPATIKANANJI WA KATIBA MPYA

Kwa kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote wanaotaka kushiriki katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ambazo zote zinapatikana
katika tovuti ya Tume ambayo ni www.katiba.go.tz

Kusoma Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba ya sasa ubora na upungufu wake na kuelewa utaratibu na masharti yanayoainishwa kisheria kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.

MAMBO YA KUZINGATIA

Kwa kuwa uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa na kusimamiwa na Sheria, Tume inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:

(a) Nani Mwenye Haki ya Kushiriki:

Mtu yeyote ambaye ni Mtanzania kwa uraia wake anayo haki ya kushiriki katika mchakato huu. Mtu ambaye kwa asili yake ni Mtanzania, lakini amepoteza uraia wa Tanzania hatoweza kushiriki; na akifanya hivyo atakuwa ametenda kosa chini ya
Sheria.

(b) Utaratibu wa Utoaji Maoni:

Njia tatu za ukusanyaji wa maoni zitatumika. Njia hizo ni kama zifuatazo:

  1. utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti (www.katiba.go.tz) barua pepe ya Tume, ( This e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it ), nukushi + 255-22-2133442 na +255-224-2230769 na
  2. utoaji wa maoni kupitia nyaraka na barua zitakazotumwa kwa Tume kutumia anwani ya Tume, ambao ni: Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681 DSM au Ofisi ndogo ya Tume, S.L.P. 2775 Zanzibar.
  3. kuhudhuria mikutano ya kukusanya maoni iliyoandaliwa na Tume (endapo Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania wakati wa ukusanyaji wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama Watanzania wengine walioko nchini).

(c) Utambulisho wa Mtoa Maoni:

Kila mtu atakayetoa maoni yake Tume anapaswa kubainisha mambo yafuatayo:-

(i) majina yake matatu;
(ii) namba ya pasi yake ya kusafiria na mahali ilipotolewa;
(iii) nchi na mji anaoishi;
(iv) endapo atatumia nyaraka au barua, ataambatanisha kivuli cha pasi yake
(ukurasa unaoonyesha maelezo ya mtu mwenye pasi hiyo).

Tume inapenda kuwakumbusha tena Watanzania kuwa utoaji wa maoni ni jambo la uhuru na hiari ya mtu na kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unawahusu raia wa Tanzania pekee.

“TOA MAONI, TUPATE KATIBA MPYA”

Last Updated ( Friday, 09 November 2012 )
 
< Prev   Next >
© 2018 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.