News Flash

On his last day in Tanzania, President Clinton became one of 360, 000 visitors annually to explore the World Famous Ngorongoro Crater. Often called "Africa’s Eden" and the "8th Natural Wonder of the World," this collapsed volcano (a “caldera”) is located in the Ngorongoro Conservation Area . This is a natural sanctuary for thousands of birds, insects and animals such as lions, zebra, black rhino and wildebeest, all free to wander.
 
Home arrow Tanzanians arrow Announcements arrow HIFADHI YA JAMII - DIASPORA (WESTADI)
HIFADHI YA JAMII - DIASPORA (WESTADI) Print E-mail

 Kwa Jumuia ya Watanzania,

Ubalozi  wa Tanzania, Sweden, umepokea barua kutoka Wizara yetu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikitufahamisha kuhusu kuanzishwa kwa huduma ya HIFADHI YA JAMII KWA WATANZANIA WAISHIO NJE – Welfare Scheme for Tanzanians in the Diaspora (WESTADI).

Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) sasa imepanua huduma zake kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupitia Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora). Lengo la bima hii ni kuondoa adha kubwa inayoipata Diaspora kuhudumia ndugu wanapougua Tanzania, au diaspora anapougua akiwa likizo Tanzania na Mtanzania anapofariki akiwa nje ya nchi.

Chini ya WESTADI, mwanachana atatakiwa kulipa ada ya dola za Kimarekani mia tatu (USD 300) kwa mwaka ili kupata mafao kama ifuatavyo;

  1. Huduma va matibabu kwa wategemezi wanne (4) wa Mwanachana ambao
    wanaishi nyumbani (Tanzania);
  2. Huduma ya matibabu kwa Mwanachama pindi atakaposafiri kuja Tanzania
    wakati wa likizo au kwa sababu zozote zile;
  3. Huduma za kusafirisha mwili wa Mwanachama kuja nyumbani iwapo atafariki
    akiwa nje ya nchi pamoja na kulipia tiketi ya msindikizaji mmoja.
  4. Huduma ya mazishi katika nchi anayoishi Mwanacharna ikiwa amechagua kuzikwa nchi aliyopo.

Mtegemezi atachagua hospitali iliyo ndani ya mkoa husika na huduma kwake zitaanza mara moja baada ya kuthibitishwa kwa ingizo la pesa za Bima ya Mtu aliyeko nje.

Huduma zitasimama mara punde mwenye bima atakapositisha na kuondoa michango ya pesa za kila mwaka.

Ili kufahamu zaidi juu ya suala hili tafadhali rejea taarifa ya uzinduzi wa WESTADI uliofanyika Septemba 2011 wakati wa Kongamano lililoandaliwa na Watanzania waishio, Dikota, Marekani bofya (HAPA).  Mgeni wa heshima katika uzinduzi huu alikuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Maelezo zaidi juu ya Mfuko huu na namna ya kuwa mwanachama yako katika tovuli ya NSSF (http://www.nssf.or.tz).

Pia kwa taarifa ya mfano kuonyesha faida ya mfuko huo kwa wanachama wake bofya hapa. (HAPA)


Ukipata taarifa hii tafadhali mfahamishe na mwingine.

UBALOZI WA TANZANIA
SWEDEN
 

Last Updated ( Thursday, 09 August 2012 )
 
< Prev   Next >
© 2019 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.